- 1,885 viewsDuration: 2:05Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya ambaye pia ni mwanachama wa muungano wa upinzani amesema kuwa muungano huo umeanzisha harakati za kumteua kinara mmoja atakayemenyana na Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza baada ya kuwapokea wazee kutoka jamii ya Agikuyu, Natembeya alisema kuwa muungano huo unaendelea kushirikisha kikosi cha Linda Mwananchi pamoja na viongozi wengine wa kisiasa ili kuunda upinzani dhabiti utakaoleta ushindani mkubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.