- 240 viewsTume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) imewaonya wanasiasa dhidi ya kutoa matamshi ya chuki na ukabila kufuatia matamshi ya hivi karibuni ya Katibu wa chama cha UDA Hassan Omar. Mwenyekiti wa tume hiyo, Dkt Kepha Omaye, amesema kumekuwa na ongezeko la matamshi ya aina hiyo nchini na akaonya kuwa tume itachukua hatua bila upendeleo dhidi ya wahusika.