Ndege za Israel zashambulia kwa mabomu Gaza, 109 wauawa

  • | VOA Swahili
    515 views
    Ndege za kivita za Israel zilishambulia kwa mabomu Gaza Ijumaa (Desemba 1) baada ya mazungumzo ya kuongeza muda wa siku saba za sitisho la mapigano na Hamas kuvunjika, ikisababisha Wapalestina waliojeruhiwa kufikishwa hospitali na wengine mitaani kutafuta hifadhi sehemu salama. Maeneo ya mashariki ya Khan Younis huko kusini mwa Gaza yalikumbwa na mashambulizi ya mabomu mara baada ya sitisho la mapigano kumalizika alfajiri, huku moshi mkubwa ukisambaa angani, waandishi wa Reuters katika mji huo walisema. Maafisa wa Afya Gaza waliripoti kuwa watu 109 wameuawa na darzeni wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo ya anga ambayo yalipiga nyumba nane. - Reuters #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF