Skip to main content
Skip to main content

Ndindi Nyoro asisitiza bei ya mafuta haipasi kuongezeka nchini

  • | Citizen TV
    456 views
    Duration: 1:29
    Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, ameitaka serikali na mamlaka ya udhibiti bei ya petroli EPRA kuhakikisha bei ya mafuta haziongezeki, akibainisha kwamba mafuta iliyoko nchini ilinunuliwa kabla ya kupanda kwa bei za kimataifa. Akizungumza katika eneo la kahuro wakati wa ufunguzi rasmi wa ofisi ya naibu kamishna wa kaunti, nyoro alisema hakuna sababu ya kuongeza bei ya mafuta kwa sasa. Nyoro pia alishutumu serikali kwa kutumia mivutano ya kimataifa, ikiwemo migogoro inayohusisha iran na marekani, kama kisingizio cha kupandisha bei ya mafuta, akionya kuwa ongezeko kama hilo litaongeza gharama za maisha kwa raia.