Skip to main content
Skip to main content

Ndovu 14 wafariki kwa sumu Kimana

  • | Citizen TV
    2,829 views
    Duration: 3:00
    Takriban ndovu 14 wameripotiwa kufariki katika Hifadhi ya Wanyamapori ya Kimana, iliyoko karibu na Hifadhi ya Taifa ya Amboseli, baada ya kudhaniwa kuathiriwa na kemikali zenye sumu kutoka kwenye mashamba ya wakulima. Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Kenya (KWS) limesema linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo, huku likitoa tahadhari kwa wasimamizi wa hifadhi zilizo karibu na Kimana kuongeza uangalizi ili kuzuia matukio kama hayo. Brenda Wanga amerejea kutoka Amboseli na anaarifu zaidi.