Ndovu watatu wauawa Olgira Kajiado Kusini baada ya kumuua mtoto

  • | Citizen TV
    6,326 views

    Ndovu watatu wameuawa katika eneo la Olgira huko Kajiado kusini na wakazi waliokuwa na gadhabu baada ya mtoto wa miaka miwili kuuwawa na ndovu na waliomwacha mamake na majeraha mabaya. Wakazi waliokuwa na hasira walianza kuwawinda ndovu hao na kuwaua wawili kwa kuwadunga mikuki huku mwingine mmoja akiuawa kwa kupiga risasi na maafisa wa KWS kama njia ya kuzuia ndovu huyo kuendeleza desturi ya kuua watu.