Ndugu wawili wafariki kutokana na kipindupindu Thika, Kiambu

  • | Citizen TV
    1,056 views

    Ndugu wawili wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika kijiji cha Komo huko Thika kaunti ya Kiambu. Francis Karanja mwenye umri wa mika 42 na kakake Stephen Njoroge mwenye umri wa miaka 52 wanakisiwa kupata ugonjwa huo baada ya kula samaki waliovuliwa kutoka kijito kichafu cha Komo kijijini humo. kulingana na msimamizi wa hospitali ya Thika Level Five Daktari Robert Muchina, wawili hao walipimwa na kupatikana na kipindupindu kabla ya kufariki walipokuwa wakipokea matibabu. Maafisa wa afya wanafuatilia kisa hicho ili kuzuia msambao wa maradhi hayo hatari