Ngoja Ngoja ya Shakahola: Familia za jamaa waliotoweka bado wanadai majibu

  • | Citizen TV
    1,736 views

    Ni matukio yaliyoanza kama taarifa za vifo vya watoto wawili waliofariki baada ya kukosa kula na kunywa, na kisha kugeuka kuwa jinamizi la mauaji ya halaiki. Watu 400 wakifukuliwa kutoka msitu wa Shakahola, kutokana na kujiunga na itikadi potofu za kidini. Na licha ya zaidi ya familia 600 kutoa msimbojeni wa vipimo kuwatafuta jamaa zao, baadhi ya jamaa sasa wanasema uchunguzi huu umechukua muda mrefu. Francis Mtalaki ana mengi kwenye makala yetu maalum kuhusu mauaji ya Shakahola.