NHIF yaongeza maradufu gharama ya maegesho

  • | Citizen TV
    2,315 views

    Kamati ya bunge kuhusu Uwekezaji inayoendesha uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa taratibu za utoaji wa mikopo, na kuongezeka kwa gharama ya mabilioni ya pesa kwenye mradi wa ujenzi wa maegesho ya hazina ya bima ya afya inataka shirika hilo la serikali kueleza jinsi Gharama ya ujenzi wa maegesho hayo hapa jijini Nairobi ilipanda kwa takriban asilimia 340. NHIF ilitumia shilingi bilioni 3.9 kujenga eneo la maegesho ambalo lilikuwa limetengewa shilingi milioni 900.