Ni afueni kwa wakulima wa pamba huko Busia baada ya kupata bei bora ya pamba yao

  • | Citizen TV
    192 views

    Wakulima wa pamba katika kaunti ya Busia wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kiwanda cha kutengeneza bidhaa za pamba cha Rivertex kuahidi kuwa kitanunua kilo moja ya bidhaa hiyo kwa bei mpya ya shilingi 72. Ni tangazo lililotolewa wakati wa mkutano wa kuandikisha mkataba wa makubaliano kati ya kiwanda cha Rivertex, mamlaka ya afya, serikali ya kaunti na wakulima.