'Niliolewa kuiokoa familia yangu'

  • | BBC Swahili
    858 views
    Karibu theluthi mbili ya ndoa za watoto zinatokea katika maeneo yenye athari kubwa za mabadiliko tabianchi, hii ni kwa mujibu wa shirika la Save the Children. Jamii zisizojiweza katika nchi hizi ziko hatarini kuingizwa zaidi katika umaskini kutokana na matukio mabaya ya hali ya hewa, na ndoa za watoto zinaoneka kama njia ya kupunguza idadi ya watu wa kutunza. Katika wilaya ya Mangochi, Malawi, ambayo inakumbwa na ukame wa mara kwa mara, baadhi ya familia zinazotegemea uvuvi na kilimo wanasema hawana chaguo lingine zaidi ya kuwaoza watoto wao. Anne Okumu ametuandalia taarifa hii; - - #bbcswahili #malawi #mimbayautotoni #mimbazautotoni #wanawake Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw