'Nilitamani kuwa injinia lakini sikuweza kuendelea na masomo' - Mwalimu Pangoma

  • | BBC Swahili
    503 views
    Baada ya kukabidhiwa darasa lenye wanafunzi zaidi ya 240, Yusuph Pangoma alianza mbinu za kuwafundisha wanafunzi hao ambao wengi walikuwa wakizungumza lugha mama (Kikurya) na hawakua wanajua kusoma, kuhesabu wala kuandika. Miongoni mwa mbinu alizobuni ni kufundisha kwa kutumia nyimbo, michezo pamoja na unyumbufu wa mwili. Mbinu ambayo imempa umaarufu na Serikali kupitia wizara ya elimu tayari imetambua kazi anayoifanya Yusuph Pangoma Mwandishi wa BBC @eagansalla_gifted_sounds ameandaa taarifa hii. #bbcswahili #Tanzania #elimu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw