Njenga na viongozi wa Azimio wanadai kuwa yanayomkumba ni vita vya kupigania kuongoza mlima Kenya

  • | K24 Video
    498 views

    Imekuwa siku ya heka heka katika makao makuu ya upelelezi wa jinai, baada ya maafisa kumzuia kwa muda aliyekuwa kiongozi wa kundi la Mungiki lililoharamishwa, Maina Njenga. Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Maina Njenga waliokuwa wamekusanyika katika makao makuu hayo. Njenga na viongozi wa Azimio wanadai kuwa yanayomkumba Njenga ni vita vya kupigania kuongoza mlima Kenya.