Nuru ya Mashariki 23-02-2026
China yaongeza kasi ya mpito kuelekea nishati ya kijani mwaka 2025
///
Mkuu wa Mawazi nchini Kenya, Musalia Mudavadi asema kuwa China ni Mwakilishi Mkuu wa Nchi za Kusini.
///
Teknolojia ya Mpunga wa Ratoon Yaimarisha Usalama wa Chakula Malaysia.
///
China imeongeza kasi ya mpito wake kuelekea nishati ya kijani mwaka 2025, huku sekta ya nishati ya jua ikiongoza ongezeko kubwa la uzalishaji na mapato ya nishati safi.
Takwimu mpya zinaonyesha mafanikio makubwa katika upanuzi wa uwezo wa umeme wa photovoltaic na mchango unaokua wa nishati safi katika uchumi wa taifa hilo.
///
Mkuu wa Mawaziri nchini Kenya, Musalia Mudavadi amesema kuwa China ni sauti imara inayowakilisha Ulimwengu wa Kusini (Global South), na akatoa salamu za Mwaka Mpya kwa China na jamii ya Wachina duniani kote wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa Kichina. Tom Wanjala na maelezo zaidi.
///
Teknolojia ya Mpunga wa ratoon kutoka China sasa inatumika nchini Malaysia kuongeza mavuno na kuimarisha usalama wa chakula, hatua inayofungua fursa mpya kwa kilimo cha maeneo ya tropiki.Jacob Mogoa anaripoti zaidi.
///
China imeanzisha kilimo cha kisasa cha mimea cha ghorofa 20 mjini Chengdu, Sichuan, chenye lengo la kuleta mapinduzi katika sekta hiyo kwa kutumia teknolojia ya kiotomatiki na mifumo ya kiviwanda.
Mradi huo unaashiria mwelekeo mpya wa kilimo cha kisasa kinacholenga kuongeza uzalishaji, ufanisi na usalama wa chakula.Khamis Darwesh anaripoti zaidi.
///
Matumizi ya teknolojia ya kisasa kama ndege zisizo na rubani na mifumo ya data yamebadilisha kilimo cha machungwa katika kijiji cha Fucheng, Chongqing nchini China, yakiongeza uzalishaji, kupunguza gharama na kufungua masoko ya kimataifa.
Simiyu Wanjala ana kina cha taarifa hiyo.
///
Ifahamu China
Kwenye sehemu yetu ya Ifahamu China leo Zakia Peng anatufahamisha jinsi China imejenga mfumo wa kina wa huduma kwa nchini humo katika Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021–2025) ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha huduma jumuishi kwa wazee.
///
Jifunze Kichina
Naam, mtazamaji, sasa ni wakati wa sehemu yetu ya Jifunze Kichina! Katika sehemu hii, tunawaletea masomo ya lugha ya Kichina, hatua kwa hatua, kwa njia rahisi na ya kuvutia. Karibu tujifunze pamoja.
Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.'
*About TV47*
'TV47 is on GOtv (Channel 102), DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES.
__
For Breaking News, kindly subscribe by sending ‘NEWS’ to 22047.
__
Connect with us:
Website: https://www.tv47.digital/
Facebook: https://www.facebook.com/TV47KE
Twitter: https://twitter.com/tv47news
Instagram: https://www.instagram.com/tv47ke/
TikTok: https://www.tiktok.com/@tv47_ke
Telegram: https://t.me/tv47_ke
WhatsApp: 0797 047 047
__