Skip to main content
Skip to main content

Nuru ya Mashariki | 27.02.2026

  • | TV 47
    27 views
    Duration: 21:39
    Nuru ya Mashariki | 27/02/2026 /// China yasajili kampuni mpya milioni 1.13 katika sekta za teknolojia na viwanda vya baadaye, mwaka 2025 /// Sekta ya rejareja ya China ilirekodi ukuaji imara wakati wa likizo ya mwaka mpya /// Marubani Vijana wa China Wakumbatia Uchumi wa Anga ya Chini /// China imeendelea kuonyesha kasi kubwa ya ukuaji katika sekta nane zinazoibukia na tisa za baadaye, ambapo takribani kampuni milioni 1.1 zilisajiliwa katika sekta hizo mwaka 2025. Hii ni ongezeko la asilimia 9.9 ikilinganishwa na mwaka uliopita, kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa Alhamisi. Tom Wanjala na maelezo kamili. /// (Mwaka Mpya wa Kichina), huku wastani wa mauzo ya kila siku ya makampuni makubwa muhimu ya rejareja ukiongezeka kwa asilimia 24 ikilinganishwa na mwaka uliopita, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka Chama cha Wafanyabiashara cha China. Khamis Darwesh anaripoti. /// Timu ya 12 ya madaktari kutoka China nchini Malawi imeendelea kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa pamoja na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya wa ndani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mfumo wa afya wa taifa hilo la Afrika.Jacob Mogoa /// Katika mji wa Chengdu, kusini magharibi mwa China, mwanamume asiyeona amewekeza akiba yake yote kuanzisha kundi la muziki linalowapa watu wenye ulemavu wa macho matumaini, urafiki na nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kama anavyoarifu Simiyu Wanjala. /// Sekta ya ndege zisizo na rubani nchini China inaendelea kukua kwa kasi, huku vijana wakichukua nafasi ya mbele katika kuendeleza uchumi wa anga ya chini. Kupitia majaribio na ubunifu wa kiteknolojia, timu ya marubani vijana katika Jiji la Kunshan inaonyesha uwezo mkubwa wa China katika tasnia ya drone ndani na nje ya nchi.Ronald Mutie anaripoti. /// China imejenga mfumo wa kina wa huduma kwa wazee na kupanua uungaji mkono kwa wazee nchini humo katika Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021–2025) kama sehemu ya juhudi za kuhakikisha huduma jumuishi, ushiriki wa kijamii na maisha rafiki kwa wazee. Mpango huo umeimarisha upatikanaji wa huduma muhimu na kuboresha ustawi wa wazee kote nchini. Jifunze Kichina Katika sehemu hii, tunawaletea masomo ya lugha ya Kichina, hatua kwa hatua, kwa njia rahisi na ya kuvutia. Karibu tujifunze pamoja. Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.' *About TV47* 'TV47 is on GOtv (Channel 102), DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES. __ For Breaking News, kindly subscribe by sending ‘NEWS’ to 22047. __ Connect with us: Website: https://www.tv47.digital/ Facebook: https://www.facebook.com/TV47KE Twitter: https://twitter.com/tv47news Instagram: https://www.instagram.com/tv47ke/ TikTok: https://www.tiktok.com/@tv47_ke Telegram: https://t.me/tv47_ke WhatsApp: 0797 047 047 __