Obunga, Plateau Queens taji la Safaricom Chapa Dimba

  • | Citizen TV
    586 views

    Obunga FC kutoka Nyanza ndio mabingwa wa makala ya nne ya Safaricom Chapa Dimba baada ya kuwarindima Pasc Langa kutoka bonde la ufa kupitia mikwaju ya penalti. Kufuatia sare ya moja moja kwenye mda wa kawaida, Obunga waliibuka mabingwa baada ya kushinda mikwaju 4-2. Upande wa wasichana Plateau Queens nao walihakikisha kuwa ubingwa wa kitaifa unasalia Nyanza baada ya kuwatitiga Barcelona Ladies mabingwa wa eneo la kati kwa mabao 5-0. Washindi wametunukiwa shilingi milioni moja huku waliomaliza wa pili wakiridhika na shilingi nusu milioni huku kikosi cha wachezaji 32 kitapiga kambi nchini uhispania kwa mazoezi ya kunoa vipaji vyao