- 864 viewsKinara wa chama cha ODM, Oburu Oginga, amesema kuwa atatetea kiti chake cha seneti katika kaunti ya Siaya, huku mwenyekiti wa chama hicho Gladys Wanga akitangaza azma yake ya kuendelea kuhudumu kama gavana wa kaunti ya Homa Bay. Haya yanajiri wakati ODM ikiweka mikakati ya kuongeza umaarufu wake mashinani ili kuvuna pakubwa katika uchaguzi ujao. Chama hicho cha Orange pia kimesema kuwa kitahakikisha kura za mchujo zinaandaliwa kwa uwazi na haki kwa wagombea wote.