OCS wa Nyahururu ajipata matatani kwa kupendekeza wanawake wachache waajiriwe katika idara ya polisi

  • | Citizen TV
    13,066 views

    Kauli ya afisa mmoja wa ngazi ya juu wa polisi ya kumtaka Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja asitishe uajiri wa wanawake katika idara ya polisi imezua hasira kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotaja semi hizo kama ubaguzi na ukiukaji mkubwa wa katiba. OCS wa Kituo cha Polisi cha Nyahururu, Isaac Kimutus alidai kuwa wanawake katika idara ya polisi wanatatiza kufanikishwa kwa kazi ngumu za polisi. Mary Muoki anazamia suala hilo linalotajwa kama dharau kwa wanawake na kauli za kuwadhalilisha.