ODM yaingia serikalini

  • | Citizen TV
    10,146 views

    Baada ya ngoja ngoja ya zaidi ya juma moja baada ya kuteuwa watu 11 kujiunga na baraza la mawaziri, Rais Ruto leo ameonekana kuzidi kujaza baraza lake la mawaziri, mara hii akionekana kuonyesha kile alichokitaja kama baraza pana la mawaziri. Rais Ruto leo akionekana kujumuisha wandani wa kinara wa upinzani Raila Odinga kwenye serikali yake.