- 15,665 viewsDuration: 7:19Chama cha ODM kinajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu bila aliyekuwa kinara wake wa muda mrefu Raila Odinga kwa mara ya kwanza tangu chama hicho kuanzishwa. Hali hiyo inayofungua mjadala kuhusu uongozi wa baadaye na uwezo wa chama hicho kuwa na usemi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao. Mjadala umeibuka kuhusu chama hicho kumezea mate kiti cha naibu rais na haswa ni nani atakayependekezwa kushikilia nafasi hiyo iwapo muungano wake na UDA utasalia. Walter Nyambaga anaangazia changamoto zinazoikabili ODM na kukiweka chama hicho kwenye mizani ya siasa za kitaifa.