- 1,213 viewsDuration: 1:34Chama cha ODM kinasema kimeanza mikakati ya kujipanga kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Kinara wa chama hicho Oburu Odinga na katibu wa chama hicho Edwin Sifuna wanasema wako tayari kufadhili mgombea wa urais atakayepeperusha bendera ya chungwa, Sifuna akipuuzilia mbali madai ya Rais William Ruto kuwa upinzani hauna makali ya kumenyana naye baada ya kifo cha hayati Raila Odinga. ODM vilevile inashikilia kuwa itaendelea kuwapigia debe wagombea wake kwenye chaguzi ndogo kote nchini.