Ofisi ya Mkuu wa Sheria imechapisha nakala ya sheria

  • | Citizen TV
    1,942 views

    Kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 28, afisi ya mkuu wa sheria kwa ushirikiano na tume ya sheria ya Kenya imechapisha nakala ya sheria za Kenya kama notisi ya kisheria nambari 221 ya mwaka 2023. Hii ikiwa ni kulingana na vipengee vya sheria ya taifa hili. Ndani ya Nakala hiyo kuna mabadiliko ya sheria ya tangu mwaka 1995 hadi 2022. Hatua hii ina ainisha sheria za Kenya na ajenda ya serikali ya Kenya Kwanza kuhusu swala nzima la Wakenya kupata taarifa wanayohitaji. Uchapishaji wa nakala hii utawasidia wakenya kupata fursa ya kutangamana na sheria zilizopo kwa urahisi mbali na kutoa nafasi ya sheria kupatikana kwa njia ya kidijitali. Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na Rais William Ruto na Mkuu wa Sheria Justin Muturi.