Ofisi za wabunge katika jumba la KICC zafungwa

  • | Citizen TV
    4,042 views

    Wabunge hii leo walijipata kwenye njia panda baada ya kukuta ofisi zao zilizoko katika jumba la KICC zimefungwa. Hatua hiyo ilitokana na malimbikizi ya kodi ya mamilioni ya pesa ambayo bunge haijalipa usimamizi wa KICC. Wabunge waliokuwa wamefika KICC kuingia ofisini walilazimika kurudi nyumbani kwani kicc imesema kuwa afisi hizo zitasalia kufungwa hadi pale tume ya huduma za bunge itakapolipa deni hilo.