Skip to main content
Skip to main content

Ongezeko la wagonjwa kutoka Uganda laibua changamoto Busia

  • | Citizen TV
    131 views
    Duration: 2:04
    Hospitali ya Rufaa ya Busia inazidi kukadiria hasara maradufu kutokana na ongezeko la wagonjwa kutoka nchi jirani ya Uganda na humu nchini wanaoshindwa kulipa bili za matibabu. Akizungumza na wanahabari mjini Busia, naibu gavana wa Busia ambaye pia ni waziri wa Afya kaunti hiyo Arthur Odera, amesikitika kuwa idara ya afya imelazimika kusamehe wadaiwa wa zaidi ya shilingi 500,000 tangu mwezi Januari kutokana na wagonjwa wengi kushindwa kulipa gharama zao za hospitali.