Operesheni ya komesha uhalifu kaskazini mwa Bonde la Ufa

  • | K24 Video
    35 views

    Bunduki haramu 148 zimenaswa na maafisa wa polisi katika kaunti sita za kaskazini mwa bonde la ufa ambako operesheni ya komesha uhalifu inaendelea. Bunduki 96 kati ya hizo zimesalimishwa leo katika kaunti ya Samburu wakati waziri wa usalama kithure kindiki alipozuru kaunti hiyo kufuatilia operesheni ya kukabiliana na wezi wa mifugo. Naibu Chifu mmoja katika eneo hilo amesimamishwa kazi baada ya mifugo walioibwa kupatikana nyumbani kwake