Operesheni ya usalama kaunti za Isiolo na Samburu

  • | KBC Video
    231 views

    Katika hatua inayolenga kusitisha operesheni ya usalama katika kaunti za Samburu na Isiolo, waakilishi wadi katika kaunti hizo wameanzisha kampeni ya kurejesha mifugo walioibwa katika eneo hilo. Kufikia sasa ng’ombe 16 wamepatikana huku wakazi wakihimizwa kusalimisha ng’ombe wowote walioibwa. Waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki aliorodhesha Isiolo, Samburu na baadhi ya maeneo ya Meru kuwa yanayolengwa katika operesheni ya Maliza Uhalifu huku vita dhidi ya ujangili na wizi wa mifugo vikizidi kupamba moto nchini.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive