- 346 viewsDuration: 15:37Zaidi ya miezi sita imepita tangu Uchaguzi Mkuu ufanyike Zanzibar, huku upinzani ukiwa bado haujajiunga na Serikali kama ambavyo Katiba ya visiwani humo inavyoelekeza. Wakati chama cha ACT Wazalendo ambacho ndicho chenye sifa ya kuunda serikali na chama tawala cha CCM - kinasisitiza kwamba wanataka madai yao kutimizwa kwanza kabla hawajaingia serikalini, CCM inasema haitaburuzwa na kwamba watatanguliza maslahi ya chama chao katika majadiliano yanayoendelea hivi sasa. ACT Wazalendo hawajaweka wazi madai yao ni yapi hasa. Mwandishi wa BBC Sammy Awami amezungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu wa Visiwani humo Othman masoud Othman 🎥: Frank Mavura #bbcswahili #tanzania #ACTWazalendo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw