Pacha wawili bado hawajajiunga na sekondari

  • | Citizen TV
    413 views

    Miezi miwili baada ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kcpe mwaka jana kujiunga na kidato cha kwanza, pacha wawili kutoka kijiji cha shauri moyo eneo la shimba hiils kaunti ya kwale wamesalia nyumbani kw akukosa karo. Gift wambua na joyce mumbe waliteuliwa kujiunga na shule za upili za shimo la tewa na kaya tiwi baada yakupata alama 343 na 287 mtawalia lakini wamesalia nyumbani kwa kukosa namna. Pacha hao wanaoishi na nyanya yao wanahofia kutoweza kutimiza ndoto zao kardi muda unavyozidi kusonga bila ya wao kusajiliwakatika kidato cha kwanza