Skip to main content
Skip to main content

Panya wavamizi wawapa msongo wa mawazo Wakulima Australia

  • | BBC Swahili
    9,521 views
    Duration: 37s
    Janga la panya linawatisha wakulima katika maeneo makubwa ya Australia huku panya hao wakienea kwa wingi karibu na nyumba na kuharibu mashamba ya nafaka. Wakulima wanasema wanaweza kuwasikia panya usiku wakikimbia kwenye dari za nyumba na ndani ya mifumo ya viyoyozi. Idadi ya panya imeongezeka kwa kasi baada ya mavuno mazuri yaliyofuatiwa na mvua za majira ya joto, hali iliyosababisha kuwepo kwa chakula kingi kwao. Hali hii inatokea wakati wakulima tayari wanakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa mafuta na mbolea kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran. Robert Kiptoo na taarifa zaidi 🎥: Brian Mala #bbcswahili #australia #panyaaustralia Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw