- 17,796 viewsDuration: 29sKiongozi wa kanisa Katoliki Papa Leo amesema ataendelea kupinga dhidi ya vita vya Marekani nchini Iran vilivyoanzishwa na Rais Trump pamoja na sera zake za uhamiaji. Hii ni baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kumkosoa moja kwa moja kiongozi wa Kanisa lenye waumini bilioni 1.4. Akizungumza akiwa ndani ya ndege ya kipapa kuelekea Algeria, ambako Papa huyo wa kwanza kutoka Marekani ameanza ziara ya siku 10 katika nchi nne za Afrika, pia alisema kwamba ujumbe wa Kikristo “unatumika vibaya.” #bbcswahili #PapaLeo #DonaldTrump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw