Passaris ataka waandamanaji kuzuiwa kufika bunge na ikulu

  • | Citizen TV
    4,775 views

    Mwakilishi wa kike wa Nairobi Esther Passaris ametetea mswada wake wa kurekebisha sheria ya maandamano nchini, unaolenga kudhibiti namna maandamano yanavyofanyika. Passaris akisema mswada wake unaolenga kukaza kamba ya maandamano utazuia maafa na uharibifu wa mali. Na kama anavyoarifu Emmanuel Too, ikiwa mswada huo utapitishwa bungeni, waandamanaji watahitajika kuwa na maeneo maalum ya kuandamana.