Polisi anayeshukiwa kumuua Rex Maasai akanusha yote

  • | Citizen TV
    8,718 views

    Isaiah Murangiri Ndumba, afisa wa polisi ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya Rez Masai aliyepigwa risasi na kuwawa wakati wa maandamano ya mwaka uliopita, amekana kuwepo jijini Nairobi wakati wa maandamano hayo. Hii ni licha ya kanda za video zilizochezwa mahakamani kuonyesha alikuwa kazini na simu yake kuonyesha alikuwa katika barabara ya Uhuru highway. Afisa huyo wa polisi pia amekana kuwa na silaha yoyote siku hiyo na kusema picha zilizoonyeshwa mahakamani sio zake.