Polisi Nakuru wachunguza mauaji ya mhalifu aliyevamiwa na wakaazi

  • | Citizen TV
    733 views

    Maafisa wa usalama eneo la Nakuru Mashariki wanachunguza kisa cha mauwaji ya msimamizi wa kundi la uhalifu linalofahamika kama Mauki. Kamanda wa Polisi wa Nakuru Magharibi Edwins Ogwari amethibitisha kuwa msimamizi wa kundi hilo anayefahamika tu kama Kenito alivamiwa na kuuliwa na wakaazi baada ya kuhusika na wizi wa kimabavu eneo la Shabaab. Polisi hata hivyo wameendelea kushika doria kwenye maeneo ya Nakuru Magharibi huku wakizidi kuwasaka viongozi wa genge la uhalifu la Confirm na magenge mengine ambayo yanawahangaisha wakaazi wa Nakuru kwa kuhusika na wizi .