Polisi wa Akiba Baringo

  • | Citizen TV
    455 views

    Viongozi kutoka Kaunti ya Baringo wameibua wasiwasi mkubwa kuhusu mienendo ya polisi wa akiba maarufu NPR katika eneo hilo, wakiwashutumu kwa ulegevu wa kujibu mashambulizi ya ujambazi yaliyokithiri. Viongozi hao wanadai kuwa polisi hao wa akiba wameshindwa kuwalinda wakaazi na huku wakilaumiwa kwa kushiriki vitendo vya uhalifu ambavyo vimesababisha vifo vingi na kuhama kwa jamii. Viongozi hao wanatoa wito kwa serikali ya kitaifa kuchukua hatua mara moja kuchunguza majukumu na mienendo ya polisi hao wa akiba. Walisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na si kuchangia vurugu zinazoendelea kukumba eneo hilo.