Polisi wa maadili Iran washtumiwa kwa kumshambulia msichana mwingine

  • | BBC Swahili
    844 views
    Msichana mwenye umri wa miaka 16 inadaiwa yupo chini ya uangalizi maalumu wa madaktari kwenye hospitali ya kijeshi baada ya kudaiwa kupigwa na polisi wa maadili kwa kutovaa hijabu. Picha za CCTV zilizotolewa na mamlaka zinaonesha kijana aliyeanguka akiondolewa kwenye treni. Maafisa wanasema alizimia nakichwa chake kugonga chuma. Iran imeimarisha sheria yake ya lazima ya kuvaa hijabu baada ya maandamano makubwa kufuatia kifo cha Mahsa Amini akiwa kizuizini kwa madai ya kutovaa hijabu yake ipasavyo zaidi ya mwaka mmoja uliopita. #bbcswahili #iran #hijabu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw