Polisi waahidi kukabiliana na makundi ya vijana wahalifu Eastleigh

  • | Citizen TV
    1,557 views

    Maafisa wa usalama eneo la Eastleigh, Nairobi wamewahakikishia wafanyibiashara wa boda boda na wakazi kuwa watakabiliana na makundi ya vijana ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakazi. Katika mkutano kati ya wahudumu hao na maafisa wa usalama eneo hilo, wafanyibiashara wamesema wameridhishwa na hatua zilizochukuliwa zikiwemo kukamatwa kwa vijana 99 ambao wanadaiwa kujihusisha na uhalifu katika eneo hilo.