Polisi katika kata ndogo ya Nyansancha eneo bunge la Nyaribari Chache, Kaunti ya Kisii, wanachunguza kisa ambapo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13 wa darasa la tisa alibakwa na kuuawa. Purity Atisia alitoweka siku nne zilizopita alipokuwa akilisha ng'ombe wao na dadake kabla ya mwili wake kupatikana katika shamba la mahindi. Babake, Nelson Atisia, anatoa wito kwa vitengo vya usalama kuharakisha uchunguzi ili waliotekeleza unyam huo waadhibiwe kisheria.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive