- 9,919 viewsDuration: 2:58Maafisa wa polisi jijini Nairobi wameanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya Daktari Victoria Nthunya Mutiso, aliyekuwa mkurugenzi katika shirika la utafiti wa afya ya akili na ubongo. Daktari huyo alipigwa risasi na kuuawa akiwa ndani ya teksi alipokuwa akielekea kazini mapema asubuhi, katika tukio ambalo wachunguzi wanashuku lilikuwa limepangwa. Polisi tayari wamemhoji mume wa marehemu pamoja na dereva wa teksi kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea kubaini waliohusika na mauaji hayo. Franklin Wallah anaripoti.