Polisi waitaka familia ya Uhuru kusalimisha bunduki

  • | Citizen TV
    6,183 views

    Familia ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta imetakiwa kusalimisha bunduki inazomiliki kwa polisi. Runinga ya Citizen imepata rekodi ya video ya maafisa waliotumwa na mweneykiti wa bodi ya kutoa leseni kwa wamiliki wa bunduki FLB Yakub Rashid akiitaka familia hiyo kusalimisha bunduki 28 anazodai inamiliki. Agizo hilo linajiri huku Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta akishikilia kuwa familia yake haina hatia kwani ilifuata taratibu zinazohitajika kupata leseni za kumiliki bunduki hizo.