Polisi wakamata washukiwa wanne wakipakia upya mbolea, mchele na mahindi mjini Nairobi

  • | Citizen TV
    1,852 views

    Polisi jijini Nairobi wamewakamata washukiwa wanne waliokuwa wakipakia upya mbolea ya ruzuku ya serikali ili kuiuza. Kulingana na kamanda wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei, pia walinasa magunia 1,360 ya mchele na mengine 200 ya mahindi ambayo yalikuwa yapakiwe upya kwenye magunia tofauti. Kulingana naye, walinasa magunia 50,000 ya mbolea katika bohari moja kwenye barabara ya Nanyuki eneo la Lungalunga hapa jijini Nairobi. Bungei amesema kwamba washukiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi ukikamilika.