Polisi walionaswa wakimpiga risasi wafika kizimbani

  • | Citizen TV
    2,420 views

    Maafisa wawili wa polisi waliohusishwa na kisa cha kupigwa risasi kwa mchuuzi wa maski siku ya jumanne jijini Nairobi wataendelea kuzuiliwa kwa siku 15 zaidi. Maafisa hao wa polisi Klinzy Masinde Barasa na Duncan Kiprono wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Capitol Hill baada ya mahakama ya milimani kuwaruhusu wachunguzi kukamilisha uchunguzi wao.