Polisi wanachunguza maauaji ya msichana wa miaka 23 huko Thika

  • | Citizen TV
    2,305 views

    Maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Thika Magharibi wanaendesha uchunguzi wa mauaji ya msichana wa umri wa miaka 23. Mwili wa Seth Njeri aliyefuzu mwaka jana ulitambuliwa katika chumba kimoja huko Thika eneo la Biafra siku ya Jumatatu. Na kama Franklin Wallah anavyorifu, uchunguzi wa maiti yake umeashiria alivyongwa na pia kudhumuliwa kimapenzi kabla ya kuuawa.