- 10,700 viewsDuration: 37sHali ya taharuki ingali imetawala eneo la tipis kwenye mpaka wa kaunti za nakuru na narok kutokana na mapigano kati ya jamii mbili. Ripoti za wakazi zikiarifu kuwa nyumba zaidi zimeteketezwa usiku wa kuamkia leo licha ya maafisa wa usalama kushika doria usiku na mchana. Wazee kutoka jamii mbili zinazozozana wamefanya mkutano wa faragha ili kutafuta suluhu ya kudumu. Kafyu iliyowekwa eneo la tipis na mwisho wa lami kwa wiki moja inaendelea kutekelezwa.