Skip to main content
Skip to main content

Polisi wanaendelea kuwasaka washukiwa wa wizi Malindi

  • | Citizen TV
    1,015 views
    Duration: 55s
    Maafisa wa polisi katika gatuzi dogo la Malindi wameendelea na msako dhidi ya magenge ya wahalifu na kufanikiwa kuwanasa washukiwa wengine 43 wa magenge hayo. Taarifa ya polisi imeeleza kuwa msako huo unafuatia ziara ya kamanda wa polisi eneo la Pwani Ali Nunow katika eneo hilo na kuwataka polisi kuongeza juhudi zao za kukabiliana na wanachama wa magenge hayo wanaoendelea kuhangaisha wananchi. Katika oparesheni hiyo iliondeshwa katika mitaa ya Karima, Soweto, Milano na Mgandini viungani mwa mji wa Malindi, washukiwa 11 wa genge la “Wakali Mwisho” walikamatwa wakiwa na simu 14 zinazoshukiwa kuwa za wizi.