Polisi wanamtafuta mwanamke aliyeiba mtoto eneo la Mwiki Kitui

  • | Citizen TV
    4,696 views

    Polisi katika eneo la Mwingi Central kaunti ya Kitui wanamtafuta mtoto wa miezi saba aliyeibwa kwenye matatu mwisho wa mwezi jana. Mama huyo wa miaka 24 kutoka eneo la Kathonzweni anasema kuwa mwanawe alitoweka na mwanamke aliyekaa naye kwenye matatu iliyokuwa ikitoka Nairobi kuelekea Kitui. Iliripotiwa kuwa, mshukiwa aliomba kumbeba mtoto wakiwa safarini kabla ya kumpuliza dawa ya usingizi. Mama ya mtoto aliamka baadaye na kufahamishwa kuwa mwanamke mshukiwa alikuwa ameshuka gari hilo eneo la magogoni akiwa na mtoto.