Polisi wanasa lita 200 za pombe haramu Mlolongo

  • | Citizen TV
    Polisi katika eneo la Mlolongo wamenasa zaidi ya lita 200 ya pombe haramu, mimea na misokoto ya bangi miongoni mwa bidhaa zingine haramu na kuwakamata washukiwa watatu. Hii ni kufuatia juhudi za hivi punde za serikali za kukabiliana na mihadarati na pombe haramu nchini Operesheni hiyo ilifanyika mjini Mlolongo na pia katika mitaa ya Kapa, Katani na Syokimau. Maafisa wa kaunti wakiandamana na machifu waliongoza shughuli hiyo. Washukiwa hao walikamatwa baada ya maafisa wa usalama kufika katika shamba moja lililoko eneo la Ngwata Phase 3. Hata hivyo mmiliki wa shamba hilo alitoroka. Wale wanaotekeleza biashara hii haramu wameonywa kuwa watakamatwa na kushtakiwa