Polisi wasema watawalinda waandamanaji Jumatano

  • | Citizen TV
    3,923 views

    Usimamizi wa kituo cha polisi cha Central umehakikishia familia za waathiriwa wa maandamano ya Juni mwaka jana kwamba maandamano ya Jumatano wiki ijayo yataendelea bila pingamizi.. Afisa anayesimamia kituo hicho cha polisi ambaye alikutana na waandalizi wa maandamano hayo amesema maafisa wake watatoa usalama kwa waandamanaji. Na kama anavyotuarifu Brenda Wanga, familia za waathiriwa zimetoa ombi la amani na kuonya dhidi ya magenge na wanasiasa kuingilia maandamano hayo