Princess wa Wales agunduliwa ana saratani, aanzishiwa matibabu

  • | VOA Swahili
    37 views
    Kate, Princess wa Wales, alisema Ijumaa ana saratani na ameanza matibabu ya chemotherapy. Hali yake ilielezwa kupitia ujumbe wa kanda ya video Jumatano na kutangazwa Ijumaa, ikiwa ni wiki kadhaa za kubahatisha kupitia mitandao ya kijamii kuhusu mahali alipo na afya yake tangu alipolazwa hospitali mwezi Januari kutokana na upasuaji wa tuboni uliokuwa haujafafanuliwa. Kate aliomba apewe “nafasi, muda na faragha yake” wakati akitibiwa kutokana na aina ya saratani iliyokuwa haijafafanuliwa. - (AP) #kate #cancer #voa