Raia wa Burundi wafurahishwa na kufunguliwa mpaka wa Rwanda.

  • | BBC Swahili
    588 views
    Raia Wa Burundi wamefurahishwa na hatua ya Serikali yao kufungua mpaka na kuwaruhusu kuingia tena nchini Rwanda. Wiki iliyopita Serikali ya Burundi ilifungua mipaka yake ya ardhini na Rwanda baada ya miaka 7 ya uhasama Wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili. Hata hivyo licha ya kufunguliwa kwa mpaka huo bado shughuli za biashara mpakani zinasuasua huku idadi ya Warundi wanaovuka ikionekana kuwa bado ni ndogo. Serikali ya Burundi inasisitiza kuwa uhusiano kamili baina ya nchi mbili utarejea hadi pale Rwanda itakapokabidhi waliotaka kufanya jaribio la kuipindua serikali ya Burundi mwaka 2015 Mwandishi wa BBC @yvesbucyana ametuandalia taarifa ifuatayo #bbcswahilileo #rwanda #burundi