Raia wa DRC aeleza faida ya uteuzi wa Bemba na Kamerhe kuwa mawaziri

  • | VOA Swahili
    610 views
    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Jean-Pierre Bemba, ambaye alikuwa gerezani kwa zaidi ya miaka 10 kwa uhalifu wa kivita, kuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo katika mabadiliko makubwa kwenye serikali. Uteuzi wake ulikuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya maafisa 57 wa serikali, ambayo msemaji wa rais alisema ni ya "haraka na lazima", katika tangazo kupitia kituo cha televisheni ya taifa ya Kongo. Rais huyo pia amemteua Vital Kamerhe, mkuu wake wa zamani wa utawala, ambaye aliachiliwa kutoka gerezani mwezi Desemba 2021 baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu, wakati alipokuwa waziri wa Fedha. Kamerhe Juni mwaka 2022 alifutiwa mashtaka yote baada ya kukataa rufaa dhidi ya mashtaka hayo. Mabadiliko hayo, ambayo yalikuwa makubwa zaidi kuliko ilivyotabiriwa, yamekuja kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Desemba 20, ambapo Tshisekedi anatarajiwa kuwania muhula wa pili. #felixtshisekedi #vitalkamerhe #JeanPierreBemba #drc #mawaziri #uteuzi #congo #voa #voaswahili #dunianileo #rais - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.